Tuesday, November 26, 2024




JESHI la Polisi mkoani Shinyanga,limewataka wananchi mkoani humo, kuwa siku ya kesho wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa,kwamba amani na usalama utakuwepo.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 26,2024, na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema kesho novemba 27 ni siku ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, kuwa Jeshi hilo limejipanga vyema kuhakikisha usalama kwa wananchi wote unakuwepo, kuanzia majumbani na kwenye vituo vya kupigia kura, na kuwasihi wananchi kwamba wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi huo sababu amani ya kutosha itakuwepo.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, tunatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, kwani tumejipanga vyema kuhakikisha usalama kwa unakuwepo muda wote kuanzia majumbani na kwenye vituo vya kupigia kura,”amesema Magomi.

Aidha, amesema Jeshi hilo pia limewakamata wahamiaji haramu Saba ambao ni Raia wa Burundi,katika kijiji cha Nyamilangano halmashauri ya Ushetu wilaya Kahama, kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria, na wamewapeleka katika ofisi za uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.

Amesema pia , wamekamata watu 51 kwa tuhuma za wizi pamoja na vielelezo mbalimbali zikiwamo bangi kilo 10, pikipiki Tisa, Pombe aina ya Moshi Lita 15,Godoro Nne, Container mbili za bati, mashine tatu za bonanza, gari likiwa na nondo 130, binding wire 11,mifuko 100 ya saruji, simu mbili, redio Saba, kabati,friji na kitanda kimoja.

Amesema kupitia kikosi cha usalama barabarani, wamefanikiwa kukamata jumla ya makosa 7,920, ambapo makosa ya gari ni 5,615, bajaji na pikipiki ni 2,305, huku wakimfikisha mahakamani dereva mmoja kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja

0 comments:

Post a Comment

Unordered List

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Duis aute irure dolor in reprehenderit in voluptate another link velit esse cillum dolore eu fugiat nulla pariatur.

Sample Text

Blog Archive

Powered by Blogger.

Search This Blog

Find Us On Facebook

Random Posts

Social Share

Flickr

Events

Text-Widgets

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis aute irure dolor in reprehenderit in voluptate another link velit esse cillum dolore eu fugiat nulla pariatur.

Sponsor

Recent comments

Recent Comments

?max-results=10">Gallery
');
    ?orderby=published&alt=json-in-script&callback=mythumb\"><\/script>");

Popular Posts

Popular Posts

Recent Posts

Header Ads

Text Widget